Home Uncategorized HAALAD ASHAURIWA KUIBUKA NDANI YA LIVERPOOL

HAALAD ASHAURIWA KUIBUKA NDANI YA LIVERPOOL


ERLING Haaland, mshambuliaji mwenye miaka 19 anayekipiga ndani ya Klabu ya Borussia Dortmund inayoshiriki Bundesliga nchini Ujerumani anatajwa kuwa kwenye rada za Manchester United na Liverpool ambao wanahitaji saini yake.

Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Norway, Jan Age Fjortof amesema kuwa sehemu bora itakayomfaa mshambuliaji huyo ni Liverpool na sio Manchester United.


Jan amesema kuwa uwezo wa mshambuliaji huyo anaweza kufiti Kwenye kikosi chochote duniani lakini sehemu pekee itakayomfaa ni Liverpool.


Haaland amekuwa akiwindwa na timu nyingi za Ligi Kuu England hivyo kubaki ndani ya Bundesliga msimu ujao nafasi inaonekana kuwa ndogo.


 “Ni mchezaji mzuri anaweza kucheza popote ila Liverpool ni bora kwake,” amesema.

SOMA NA HII  VIDEO: MASAU BWIRE, VIJANA WANACHEZA BILA MAWAZO,TUMEWAPAPASA SIMBA