Home Uncategorized BERNARD MORRISON AONGEZA IDADI YA WATAKAOUKOSA MCHEZO WA MWADUI FC

BERNARD MORRISON AONGEZA IDADI YA WATAKAOUKOSA MCHEZO WA MWADUI FC


BERNARD Morrison, anaongeza orodha ya wachezaji wa Yanga watakaoukosa mchezo wa kesho dhidi ya Mwadui FC.

Wengine ambao wataukosa mchezo huo ni pamoja na Papy Tshishimbi ambaye ni nahodha kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa bado hajawa fiti.

Ally Ally na Erick Kabamba, hawapo kwenye mpango wa sasa mpaka mchezo ujao.

Habari zinaeleza kuwa Morrison ilipaswa kwenda na Kocha leo Shinyanga ila imeshindikana kutokana na sababu ambazo hazijawekwa wazi.

“Morrison alipaswa kuondoka leo na Kocha Mkuu, Luc Eymael ila imeshindikana ndio maana ameondoka David Molinga kwenda kuchukua nafasi yake,” ilieleza taarifa hiyo.

Juni 14 Yanga itamenyana na Mwadui FC, Uwanja wa Kambarage.

SOMA NA HII  HAJI MANARA ATANGAZA KUBWAGA MANYANGA NDANI YA SIMBA