Home Uncategorized ALLIANCE FC WATANGAZA HATMA YA KOCHA WAO MALALE HAMSINI

ALLIANCE FC WATANGAZA HATMA YA KOCHA WAO MALALE HAMSINI


UONGOZI wa Alliance FC umesema kuwa kwa sasa wanamsubiri kocha wao Malale Hamsini asaini kandarasi mpya ili aendelee na kazi kwani msimu uliopita alifanya mambo makubwa.

Kwa sasa Hamsini amemaliza mkataba wake na bado hajasaini mkataba mpya kwa kile alichodai kwamba bado hajawasiliana na viongozi wa Alliance FC.

Akizungumza na Salehe Jembe, Ofisa Habari wa Alliance, Jacson Mwafulango amesema kuwa wanaamini uwezo wa Hamsini hali iliyofanya wamuandalie mkataba mapema.

“Sisi Alliance tunatambua kwamba Hamsini ni kocha wetu ndio mana tumemuandalia mkataba hivyo kilichobaki kwa sasa ni yeye mwenyewe kusaini ili kuendeleza mipango kwa ajili ya msimu ujao,” amesema.

SOMA NA HII  ZAHERA AMZUNGUMZIA KIVINGINE KABISA SAID NDEMLA, AIBUA KIOJA KWA MKAPA