Home Uncategorized JAMES KOTEI ATAJWA KUMALIZANA NA YANGA MIAKA MIWILI

JAMES KOTEI ATAJWA KUMALIZANA NA YANGA MIAKA MIWILI


INAELEZWA kuwa kiungo wa zamani wa Klabu ya Simba aliyetwaa tuzo ya kiungo bora ndani ya Simba kwa msimu wa 2018/19 amesaini kandarasi ya miaka miwili ndani ya Klabu ya Yanga.

Mpango mkubwa wa Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu Luc Eymael ni kuboresha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao hivyo wameanza na Kotei ambaye anauzoefu na ligi ya Bongo.

Kotei alipomalizana na Simba alijiunga na Klabu ya Kaizer Chief ya Afrika Kusini kwa sasa anakipiga ndani ya Klabu ya FC Slavia-Mozŕy.


Antonio Nugaz, Ofisa Uhamasishaji na Msemaji wa Yanga amesema kuwa hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa wakati wa usajili haujafika.

SOMA NA HII  BREAKING: YANGA KUMENOGA, YAMSHUSHA GWIJI ALIYEKUWA BENFICA