Home Uncategorized WAWA AIPIGA MKWARA MZITO AZAM FC

WAWA AIPIGA MKWARA MZITO AZAM FC


BEKI wa kazi wa Simba, Muivory Coast, Pascal Wawa, amebainisha kwamba licha ya ugumu ambao watakutana nao kwenye mechi dhidi ya Azam FC, hakuna ambacho kitawazuia wao kuingia nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC), maarufu kama FA.

Beki huyo ameongeza kuwa watapambana watakavyoweza kuona wanalitimiza suala la kuingia nusu fainali kwa kuwafunga wapinzani wao Azam.

Simba imepangiwa kucheza na Azam FC katika mechi ya nusu fainali ambayo imekuwa gumzo kutokana na matokeo yao kwa msimu huu. Mtanange huo utapigwa kati ya Juni 30 na Julai Mosi, mwaka huu.

Muivory Coast huyo amesema kuwa mechi hiyo haitakuwa rahisi hata kidogo kutokana na wapinzani wao nao kuwaza ushindi lakini kilichopo akilini mwao ni kushinda na kuingia nusu fainali.
“Wapinzani wetu Azam ni wazuri na tutakapokutana ushindani utakuwa mkubwa sana. Kama ambavyo imekuwa kwenye kila mechi tunayocheza nayo.
“Lakini kwetu sisi tunataka kitu kimoja tu, kushinda, tunataka kuona tunacheza nusu fainali hivyo ni muhimu kupambana na kupata matokeo mazuri,” alimaliza beki huyo.
Timu hizo zimekutana mara tatu msimu huu, Simba ikishinda zote. Mechi ya kwanza ya Ngao ya Jamii, Simba ilishinda 4-2, kisha ikashinda 1-0 kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi kabla ya kushinda tena 3-2 kwenye mechi ya mzunguko wa pili.
SOMA NA HII  UZI MPYA WA AZAM FC ACHA KABISA,AGOSTI 23 KILELE CHA AZAM FESTIVAL