Home Ligi Kuu VITA YA PIRA SPANA V PIRA BURUDANI, UHURU

VITA YA PIRA SPANA V PIRA BURUDANI, UHURU

 


LEO, Uwanja wa Uhuru kutakuwa na vita ya pira spana kutoka kwa Klabu ya KMC dhidi ya pira burudani kutoka kwa Kagera Sugar.

Ikiwa ipo nafasi ya 6 na pointi zake 28 inawakaribisha Kagera Sugar waliojichimbia nafasi ya 10 na pointi zao ni 24 wote wakiwa wamecheza jumla ya mechi 20.

 Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala alisema kuwa wapo tayari kwa ajili ya kutembeza pira spana na pira mapato mbele ya Kagera Sugar ili wavune pointi tatu muhimu.

Mecky Maxime, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar alisema kuwa wataingia uwanjani kutoa burudani na kufunga mabao kwa kuwa raha ya mpira ni kufunga na kutoa burudani.

KMC imetoka kushinda mabao 2-1 dhidi ya Mwadui FC inakutana na Kagera Sugar ambayo imetoka kulazimisha sare ya kufungana mabao 3-3 dhidi ya Yanga.

SOMA NA HII  DABI YA YANGA PRINCESS V SIMBA QUEENS KUANZA KUCHORA RAMANI YA BINGWA