Home Simba SC MASHABIKI WARUHUSIWA KUINGIA SIMBA V KAIZERS CHIEFS, SIMBA KUOMBA WENGINE ZAIDI

MASHABIKI WARUHUSIWA KUINGIA SIMBA V KAIZERS CHIEFS, SIMBA KUOMBA WENGINE ZAIDI


 KUELEKEA kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika unaotarajiwa kuchezwa Mei 22, Uwanja wa Mkapa, mashabiki wameruhisiwa kuingia ila watafanya maombi mengine ili kuruhusiwa mashabiki wengi zaidi.

Hii inatokana na kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona ambavyo bado vinaisumbua dunia kwa sasa.

Ni Simba v Kaizer Chiefs unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa ambapo ule wa awali wakati Simba ikikubali kichapo cha mabao 4-0 hakukuwa na mashabiki ambao waliruhusiwa kuingia katika mchezo huo.

Sasa Mei 22 uongozi wa Simba umesema kuwa umeruhusiwa kuingiza mashabiki ambao wamepata nafasi ya kuingia kwenye mchezo huo.

Haji Manara amesema:”Mpaka sasa tumeruhusiwa mashabiki 10,000 lakini tunaendelea kuomba kuongeza. Naomba uwanjani rangi iwe nyekundu na nyeupe,” .


SOMA NA HII  TFF YAIPA SIMBA KIPORO 'CHENGINE' ...WARUDIA MAKOSA YA MSIMU ULIOPITA WAKAFUNGWA NA KAIZER..