Home Habari za michezo TFF YAIPA SIMBA KIPORO ‘CHENGINE’ …WARUDIA MAKOSA YA MSIMU ULIOPITA WAKAFUNGWA NA...

TFF YAIPA SIMBA KIPORO ‘CHENGINE’ …WARUDIA MAKOSA YA MSIMU ULIOPITA WAKAFUNGWA NA KAIZER..


Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ limeusogeza Mbele Mchezo namba 090 wa Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ kati ya Simba SC dhidi ya Pamba SC ya Mwanza.

Mchezo huo ulikua umepangwa kuchezwa Jumatano (April 13) katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Kwa maamuzi hayo mchezo huo utapangiwa tarehe nyingine, lakini Uwanja wa Benjamin Mkapa utaendelea kuwa mwenyeji.

Sababu kubwa ya kuahirishwa kwa mchezo huo ni kuipa Simba SC muda wa kujiandaa zaidi na mchezo wa Robo Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Orlando Pirates.

Simba SC itacheza dhidi ya Orlando Pirates Jumapili (April 17), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, huku mchezo wa Mkondo wa Pili ukipangwa kuchezwa April 24 Afrika Kusini.

Hali kama hii ilitokea msimu uliopita ambapo Simba walipewa kiporo cha kwenye Ligi Kuu kwa ajili ya kupisha na kufanya maandalizi ya mchezo wa Robo fainal Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs, ambapo matokeo yake Simba waliucheza mchezo huo bila ya kuwa na utimamu na ufiti wa mechi na kupelekea kufungwa magoli manne.

SOMA NA HII  MWAMBA HUYU HAPA KUTOKA AZAM, SAHANI MOJA NA BALEKE LIGI KUU