Home Uncategorized CAF YATEUA WAAMUZI SITA WA ONGO KUCHEZESHA MECHI ZA LIGI YA MABINGWA...

CAF YATEUA WAAMUZI SITA WA ONGO KUCHEZESHA MECHI ZA LIGI YA MABINGWA NA SHIRIKISHO


SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua Waamuzi Wanne (4) na Makamishna Wawili(2) kutoka Tanzania kusimamia mechi za Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho.

Elly Sasii atasimama katikati kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa kati ya Aigle Noir ya Burundi dhidi ya Gor Mahia ya Kenya utakaopigwa Uwanja wa Prince Louis Rwagasore, Burundi Agosti 11, 2019.

Sasii atasaidiwa na Mwamuzi msaidizi namba 1 Frank Komba, mwamuzi msaidizi namba 2 Ferdinand Chacha, mwamuzi wa akiba, Emmanuel Mwandembwa na kamishna wa mchezo anatokea Rwanda, Gaspard Kayijuka.

Ahmed Mgoyi atakua Kamishna wa mchezo wa marudiano Ligi ya Mabingwa Gor Mahia dhidi ya Aigle Noir utakaochezwa kati ya Agosti 23,24 na 25 nchini Kenya.

Khalid Abdallah ameteuliwa kuwa kamishna wa mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Proline FC ya Uganda na Master Security Services ya Malawi utakaochezwa Uwanja wa Kampala Startimes nchini Uganda.

SOMA NA HII  YANGA WATAJA SABABU YA KUCHEZA MECHI ZA KIRAFIKI