Home news WANAJESHI WA MPAKANI, KAZINI LEO KIMATAIFA

WANAJESHI WA MPAKANI, KAZINI LEO KIMATAIFA


WANAJESHI wa mpakani, Biashara United leo wanakibarua cha kusaka ushindi mbele ya FC Dikhil ya Dijibout utakaochezwa Stade du Ville.

Mchezo huo utachezwa leo Septemba 10, saa 9:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki. 

Kwa mujibu wa Katibu wa Biashara United,  Haji Mtete amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo huo na watapambana kupata matokeo chanya.

“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya FC Dikhil na tunajua kwamba haitakuwa kazi rahisi tutafanya vizuri,”.

Biashara United ya Mara ni mara yao ya kwanza kushiriki mashindano ya kimataifa baada ya kumaliza ligi ikiwa nafasi ya nne.

SOMA NA HII  ACHANA NA RONALDO...HUU HAPA MCHUMA ANAOTUMIA MESSI KUPAA NAO ANGANI...NI NOMAA NA NUSU...