Home Uncategorized ALIYEMPA TABU MANULA KUREJEA KUTOKA AFRIKA KUSINI

ALIYEMPA TABU MANULA KUREJEA KUTOKA AFRIKA KUSINI


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa hali ya nyota wao kipenzi cha mashabiki, Mapinduzi Balama kwa sasa inaendelea vizuri na muda wowote kuanzia sasa anaweza kurejea Bongo.


Nyota huyo ambaye anakumbukwa kutokana na kuanza kuweka mzani sawa kwenye Dar Dabi ya mabao 2-2 dhidi ya Simba kwa kumtungua Aishi Manula bao la nje ya 18.

 

Msimu wa 2020/21 amekuwa nje mpaka wakati huu wa raundi ya 17 kutokana na kutibu majeraha yake ili aweze kuwa fiti.


Mapinduzi alipelekwa Afrika Kusini hivi karibuni kupatiwa matibabu kutokana na kuvunjika mguu tangu msimu uliopita alipokuwa mazoezini.

 

 Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa, tayari kiungo huyo anaendelea vyema na matibabu na wiki ijayo akitarajiwa kurudi hapa nchini.

 

“Mapinduzi anaendelea vizuri, tumewasiliana na madakari wake wamesema anaendelea vyema na tayari ameshafanyiwa upasuaji, wiki ijayo anatarajia kurejea nchini,” amesema Mwakalebela.

SOMA NA HII  MAXI NZEGELI AFANYA MAAJABU HAYA KIKOSINI SKUDU HAAMINI MACHO YAKE