Home Habari za michezo MCHAMBUZI:- KWA YANGA HII…KUNA TIMU ITAPIGWA GOLI 4 KWENYE DABI….

MCHAMBUZI:- KWA YANGA HII…KUNA TIMU ITAPIGWA GOLI 4 KWENYE DABI….

azam vs yanga

Wikiendi iliyopitwa wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Simba na Yanga walikuwa ugenini wakisaka nafasi ya kucheza hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa.

Yanga walikuwa nchini Rwanda katika Dimba la Kigali Pele wakiwakabili Al Merrikh ya Sudan na kufanikiwa kuondoka na ushindi wa bao 2-0.

Simba walikuwa Zambia wakikipiga na wenyeji Power Dynamos katika Dimba la Levy Mwanawasa na kulazimishwa sare ya mabao 2-2.

Baada ya mchezo huo wadau wengi wa masuala ya kandanda walionekana kuwa na wasiwasi na kiwango kilichooneshwa na Simba SC katika mchezo huo.

Miongoni mwao ni mchambuzi wa Soka toka Clouds Media Edgar Kibwana ambae anasema kuwa;

“Kuna timu kila nikiiangalia naona kabisa dabi ya Novemba watapigwa goli nne, huu mwenendo wao wasipobadilika nina uhakika watapigwa tu”.

SOMA NA HII  YANGA WABAINISHA KILICHOWAPONZA KWA MKAPA