Home Yanga SC YANGA: UBINGWA BADO HATUJAUKATIA TAMAA

YANGA: UBINGWA BADO HATUJAUKATIA TAMAA


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa bado una matumaini ya kutwaa taji la Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21 kwa kuwa hawajakata tamaa.

Ikiwa ipo nafasi ya kwanza na pointi zake ni 50 kibindoni inapewa presha na watani zao wa jadi Simba.

Simba ambao ni mabingwa watetezi wana pointi 46 wakiwa wamecheza mechi 20 huku Yanga ikiwa imecheza jumla ya mechi 23.

Mwendo wa kusuasua mzunguko wa pili baada ya kucheza mechi sita, ilishinda mechi moja, kupoteza moja na sare nne jambo lililofanya wamfute kazi, Cedric Kaze ambaye alikuwa kocha mkuu na Nizar Khalfan ambaye alikuwa ni msaidizi wake.

Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla amesema kuwa bado nia ipo na hawajakata tamaa ya kuhitaji kutwaa ubingwa.

“Ligi haijaisha mashabiki wasiwe na mashaka bado tuna nafasi ya kutwaa ubingwa na tutafanya vizuri kwenye mechi ambazo zimebaki.

“Ikiwa tutasema kwa sasa tukate tamaa itakuwa sio sawa kwani hakuna mwenye uhakika wa kulitwaa kombe mpaka pale atakapocheza mechi zake nasi bado hatujamaliza mechi zetu.

“Tangu mwanzo wakati ligi inaanza tulikuwa tunahitaji kutwaa kombe na kwa kuwa ligi haijaisha basi hakuna haja ya kuwa na mashaka,” amesema.

SOMA NA HII  SIMBA WAIKATAA YANGA...MECHI YAO YAFA KIBUDU....ISHU YA USAJILI YATAJWA....