Home Habari za michezo BAADA YA KUANZA LIGI KWA GIA KUBWA YA USHINDI…ZORAN AANZA TAMBO MSIMBAZI…ARUDIA...

BAADA YA KUANZA LIGI KWA GIA KUBWA YA USHINDI…ZORAN AANZA TAMBO MSIMBAZI…ARUDIA YA AHMED ALLY…


Achana na mchezo wa juzi, lakini kocha wa Simba, Zoran Maki amesema mashabiki wao hawapaswi kuwa na presha, kwani licha ya kufanya vibaya katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga kwa mabao 2-0, alikaa na wachezaji kuzungumza ili kuwaweka sawa kisaikolojia na kwamba mambo matamu yanakuja Msimbazi.

Akizungumza kabla ya mechi ya juzi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Geita Gold, Zoran alisema alifanya kikao na wachezaji ili wasahau yaliyopita na kufikiria kazi iliyo mbele yao katika mechi za Ligi Kuu, Kombe la ASFC na Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Nimewaweka vizuri kisaikolojia na akili zao ili kupokea vitu vya kiufundi vizuri turudi katika mechi nyingine za kimashindano tukiwa na nguvu kubwa ya kupambania matokeo mazuri,” alisema Zoran.

“Baada ya hapo niliwaeleza ligi ni kama marathoni unaweza kuanza vibaya na ukaja kumaliza vizuri, ilitokea tulishindwa kufanya vizuri katika mechi ya Yanga, basi tunatakiwa kumaliza vizuri kwa kuchukua mataji katika mashindano mengine.

“Nimewaambia nahitaji zaidi uwajibikiaji kwa kila mmoja wakitakiwa kutambua majukumu wawapo uwanjani ili kuhakikisha Simba inaonyesha ukubwa wake kwa kufanya vizuri katika mashindano.

Zoran alishukuru mazoezini wachezaji walionekana kuwa na mabadiliko kwa kufanya vile ambavyo alitaka na anaamini utamu utaendelea Msimbazi kwa vile hakuna lisilowezekana kwa namna walivyojipanga.

Baada ya mechi ya jana, Simba itasalia Dar es Salaam kuisubiri Kagera Sugar wikiendi hii kisha kumalizana na KMC kabla ya jukumu la mechi za kimataifa.

SOMA NA HII  TRY AGAIN: NTIBAZONKIZA NI MCHEZAJI MZURI....NAMPENDA..LAKINI SASA....HATUTAWAHESHIMU YANGA....