Home Habar za Usajili Simba KUELEKEA MECHI YA KESHO DHIDI YA KAGERA….MATOLA NA SIMBA YAKE WATAMBA KUNG’ANG’ANIA...

KUELEKEA MECHI YA KESHO DHIDI YA KAGERA….MATOLA NA SIMBA YAKE WATAMBA KUNG’ANG’ANIA KILELENI….


Kocha msaidizi wa Simba, Selemani Matola ameweka wazi kutokuwa na majeruhi ndani ya kikosi chake hivyo wachezaji wote wapo tayari kwa mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu kesho Agosti 20, 2022 dhidi ya Kagera Sugar kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

Matola amezungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari leo kwenye ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) huku akitamba kwenda kushinda mechi hiyo.

“Hadi sasa wachezaji wote ni wazima wa afya, hatuna majeruhi hata mmoja hivyo wote watashiriki uwanjani kama ilivyo kawaida,” amesema Matola na kuongeza;

“Mchezo wa kesho sio mwepesi ni mgumu kwani Kagera wapo imara hivyo tutajipanga na mbinu mpya kuhakikisha tunashinda na hatuwezi kutumia mbinu tulizotumia kwa Geita Gold kuwa ni timu tofauti na tumejipanga kivingine.”

Kwa upande wa wachezaji nahodha msaidizi wa Simba, Shomari Kapombe amesema hadi sasa wapo tayari kwa mchezo wa kesho na mashabiki wategemee mazuri kutoka kwao.

“Tupo tayari na mchezo huu licha ya kwamba Kagera ni timu ngumu lakini tumejipanga kupambana hadi mwisho kuhakikisha timu inapata ushindi,” amesema Kapombe.

Katika mechi za ufunguzi wa ligi kwa kila timu, Simba ilishinda 3-0 dhidi ya Geita Gold nyumbani huku Kagera ikipoteza kwa kuchapwa 2-1 na Azam ugenini.

Msimu uliopita timu hizo zilipokutana katika mchezo wa kwanza, Kagera ilishinda 1-0 nyumbani na mechi ya Marudiano Simba ikaibuka na ushindi wa 2-0 ikiwa uwanja wa Benjamin Mkapa.

SOMA NA HII  WAKATI ZIKICHEZA LEO....KMC FC WAITANGAZIA KIAMA KAGERA SUGAR