Home Uncategorized MSERBIA WA YANGA AVUNJA REKODI KIBABE

MSERBIA WA YANGA AVUNJA REKODI KIBABE

 


ZLATKO Krompotic, Kocha Mkuu wa Yanga ingizo jipya lililobeba mikoba ya Luc Eymael raia wa Ubelgiji amevunja rekodi ya pointi ndani ya kikosi hicho iliyowekwa kwa msimu wa 2019/20.

Ilipoanza kunolewa na Mwinyi Zahera ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi ndani ya Klabu ya Gwambina FC, kwenye mechi tatu za mwanzo ambazo ni dakika 270, Yanga ilikusanya pointi tano pekee.

Msimu mpya wa 2020/21 kwenye mechi tatu za mwanzo ambazo ni dakika 270 imesepa na pointi saba mazima ikiongeza pointi mbili zaidi ya msimu uliopita.

Ilianza kuyeyusha pointi tatu mbele ya Ruvu Shooting kwa kichapo cha bao 1-0 kisha ikaambulia pointi moja mbele ya Polisi Tanzania kwenye sare ya kufungana mabao 3-3 kisha ikasepa na pointi tatu mbele ya Coastal Union wakati ikishinda bao 1-0 mechi zote zilipigwa Uwanja wa Uhuru.

Msimu huu Yanga imekusanya pointi saba kwenye mechi tatu za mwanzo ambapo ilianza kusepa na pointi moja kwenye sare ya kufungana bao 1-1 na Tanzania Prisons, ikasepa na pointi tatu ikishinda bao 1-0 mbele ya Mbeya City, hizi mbili ilikuwa Uwanja wa Mkapa kisha ikashinda bao 1-0 mbele ya Kagera Uwanja wa Kaitaba.

Msimu uliopita Yanga Ilimaliza ligi ikiwa nafasi ya pili na pointi 72 kibindoni baada ya kucheza mechi 38 ambazo ni dakika 3,420.

SOMA NA HII  ORODHA HII HAPA YA NYOTA 11 WA SIMBA WATAKAOIKOSA YANGA