Home Uncategorized ORODHA HII HAPA YA NYOTA 11 WA SIMBA WATAKAOIKOSA YANGA

ORODHA HII HAPA YA NYOTA 11 WA SIMBA WATAKAOIKOSA YANGA


 LEO Uwanja wa Amaan, visiwani Zanzibar kutakuwa na mchezo wa Dar Dabi kati ya Yanga dhidi ya Simba ambao ni wa Kombe la Mapinduzi.

Yanga inakutana na Simba mara ya pili kwenye fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya ile ya kwanza kuwakutanisha msimu wa 2011. Kwenye fainali hiyo Yanga ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 na Simba.

Nyota 11 wa Simba wanatarajiwa kukosekana kwenye mchezo wa leo ambao ni pamoja na :-Clatous Chama Luis Miquissone, Rarry Bwalya walipewa mapumziko baada ya mchezo wa kimataifa dhidi ya FC Platinum.

Aishi Manula, John Bocco,Erasto Nyoni

Shomari Kapombe,Said Ndemla hawa walikuwa kwenye timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambayo jana ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya DR Congo na ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1.

Jonas Mkude yeye amesimamishwa na timu yake kwa kosa la nidhamu.

Charles Ilanfya hayupo fiti kwa kuwa hajacheza mchezo hata mmoja wa Kombe la Mapinduzi msimu wa 2021.

 Pascal Wawa beki kitasa wa Simba raia wa Ivory Coast huyu hayupo fiti anaumwa.

Kwa mujibu wa Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Seleman Matola amesema kuwa hana mpango wa kuwaongeza wachezaji waliopo kwenye kambi ya Stars.

SOMA NA HII  JACK GREALISH ANAITAMANI MANCHESTER UNITED