Home Uncategorized KOCHA COASTAL UNION AWATAKA WACHEZAJI KUCHUKUA TAHADHARI NA KULINDA VIPAJI VYAO PIA

KOCHA COASTAL UNION AWATAKA WACHEZAJI KUCHUKUA TAHADHARI NA KULINDA VIPAJI VYAO PIA

JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa ni muhimu kwa wachezaji wake kufanya mazoezi kwa sasa kujiweka sawa licha ya kupitia kipindi kigumu.

Ligi Kuu Tanzania Bara imesimamishwa na Serikali ili kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo  wachezaji wapo nyumbani baada ya kambi kuvunjwa.

Mgunda amesema:”Ni kipindi kigumu ambacho tunapitia kwa sasa ni dunia nzima inapambana lakini ni muhimu kwa wachezaji kuchukua tahadhari ili kujilinda na Virusi vya Corona pamoja na kulinda vipaji vyao kwa kufanya mazoezi,”.

SOMA NA HII  WACHEZAJI YANGA KULA CHRISTMAS MBEYA