Home Simba SC KUMBE! ONYANGO HAJUI KUHUSU KUHITAJIKA NA TIMU YA AFRIKA KUSINI

KUMBE! ONYANGO HAJUI KUHUSU KUHITAJIKA NA TIMU YA AFRIKA KUSINI


BEKI wa kati wa klabu ya Simba, raia wa Kenya, Joash Onyango amesema kwa sasa bado hajapata taarifa yeyote kuhusu yeye kuhitajika na Klabu ya Orlando Pirates ya nchini Afrika Kusini.


 Hivi karibuni imekuwa ikielezwa kuwa beki huyo yupo kwenye rada za mabosi wa timu ya Afrika Kusini wakihitaji kupata saini yake.


Kuhusu suala hilo Joash Onyango amesema; “Bado sijapata taarifa zozote kuhusu hilo.”

 

Tokea ajiunge na kikosi cha Simba mwanzoni mwa msimu huu, Onyango ameoneha kiwango bora na kuwa mlinzi chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Didier Gomes 

 

Onyango amefunga bao moja kwenye ligi kuu bara tena likiwa ni la kuisawazishia Simba kwenye mchezo dhidi ya Yanga na kuufanya mchezo uishe kwa sare ya bao 1-1 na kutengeneza nafasi moja ya bao kwa kumpasia John Bocco aliyefunga bao pekee dhidi ya klabu ya Mwadui.

SOMA NA HII  SABABU YA KIBU DENIS KUGOMEA MKATABA MPYA SIMBA...KUMBE YANGA WAMWAGA DAU NONO