Home Uncategorized HESABU KUBWA ZA SIMBA MSIMU HUU HIZI HAPA

HESABU KUBWA ZA SIMBA MSIMU HUU HIZI HAPA

JONAS Mkude, kiungo ndani ya Simba amesema kuwa akili zao kwa sasa ni kuona namna gani wanaweza kutetea taji lao la ubingwa walilotwaa msimu uliopita 2018/2019.

Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 59 kibindoni ikiwa imecheza mechi 23 kesho itamenyana na Biashara United kwenye mchezo wa ligi utakaochezwa Uwanja wa Taifa.

“Mpango mkubwa ni kuona namna gani tunaweza kutetea ubingwa wetu ambao tuliutwaa msimu uliopita, mashabiki watupe sapoti,” amesema.

Mkude ametupia mabao mawili na mguuni ana pasi mbili za mabao.

SOMA NA HII  WACHEZAJI YANGA WACHELEWESHA KUANZA KWA KAMBI