Home news CEDRIC KAZE AIBUA JIPYA YANGA…ATOA MASHARTI …AGUSIA UBINGWA NA NAMNA YANGA WANAVYOCHEZA…

CEDRIC KAZE AIBUA JIPYA YANGA…ATOA MASHARTI …AGUSIA UBINGWA NA NAMNA YANGA WANAVYOCHEZA…


Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema endapo wanahitaji kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Msimu huu 2021/22, kikosi chao kinapaswa kupambana katika viwanja vizuri na vibovu.

Kaze ametoa rai hiyo kwa wachezaji wa Yanga, baada ya kuambulia alama moja dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa mzunguuko wa sita wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Jumamosi Novemba 21 mwaka huu Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi.

Kaze ambaye alikua Mkuu wa Benchi la Ufundi klabuni hapo kabla ya kutimuliwa mwishoni mwa mwaka 2020 na kisha kurejea kama Msaidizi wa Kocha Nabi amesema:

“Kama tunahitaji ubingwa inabidi wachezaji wetu waweze kucheza kwenye viwanja vya aina zote, vizuri na vibovu, hivyo inabidi sasa tujielekeze kuwafundisha jinsi ya kucheza kwenye aina mbalimbali za viwanja, lakini pamoja na hayo tunashukuru kwa kupata pointi moja, tunakwenda kujipanga.”

Sare ya 1-1 dhidi ya Namungo FC imeifanya Young Africans kufikisha alama 16 zinazoendelea kuwaweka kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu, huku Simba SC ikifuatia kwa kuwa na alama 14.

Young Africans itarudi tena Uwanjani juma lijalo (Novemba 30), kucheza dhidi ya Mbeya Kwanza FC itakayokua nyumbani Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya, huku Simba SC ikitarajia kucheza dhidi ya Geita Gold FC, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

SOMA NA HII  BALAMA MAPINDUZI AREJEA KAZINI SASA