Home Uncategorized JEMBE LA KAZI SASA LAANZA MAZOEZI NDANI YA SIMBA

JEMBE LA KAZI SASA LAANZA MAZOEZI NDANI YA SIMBA


MZAMIRU Yassin, kiungo wa Simba ameanza mazoezi ili kurejea uwanjani kutokana na majeraha aliyoyapata kwenye mechi dhidi ya Yanga.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Januari 4 timu zote zilitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2.

Yassin akiwa na Simba kwenye mechi za Ligi Kuu Bara alihusika kwenye jumla ya pasi tatu za mabao ambapo mbili alimpa Meddie Kagere mwenye mabao 13 na moja alimpa Miraj Athuman mwenye mabao sita.

SOMA NA HII  KOCHA YANGA AFICHUA TIMU YAKE INAPOBORONGA - VIDEO