Home Habari za michezo BAADA YA KUCHAPWA JUZI…NABI AVUNJA UKIMYA YANGA…AANIKA WALIOFELISHA MIPANGO…

BAADA YA KUCHAPWA JUZI…NABI AVUNJA UKIMYA YANGA…AANIKA WALIOFELISHA MIPANGO…

Habari za Yanga SC

Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga Nasreddine Nabi ametaja sababu ya kukosa ushindi kwenye mechi ya kwanza ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger ambao ulichezwa juzi kwa Mkapa.

Yanga walichapwa mabao 2-1 kutoka kwa USM Alger na kuweka kwenye wakati mgumu wa kuchukua kombe hilo na Nabi amesema hawakupata muda wa kutosha kujiandaa kuelekea katika mchezo huo kama ambavyo ilitakiwa.

Nabi alisema maandalizi hayakuwa bora sana kama ambavyo walitakiwa kuwa nayo kwa sababu walikuwa na muingiliano wa ratiba hapa katikati na ndiyo maana imetokea hiki kilichotokea.

“Maandalizi yetu ni magumu, hatujapata muda wa kutosha, tumetumia muda mwingi kwenye ‘recovery’, tunataka tutoe wito kwa wanaoandaa ratiba tunaliwakilisha taifa, tunaomba siku zijazo lisitokee tena.

“Wachezaji walihitaji muda wa kupumzika na wakati wa kujiandaa. Hakuna namna nyingine, tunakaa na kuona tunachezaje mechi ya marudiano kwa sababu hata hivyo hatuna muda tena wa kutosha,” alisema.

SOMA NA HII  MAMELODI SUNDOWN YAWAITA SIMBA SAUZI....WAANDAA MASHINDANO YAO KWA KLABU NNE TU ZA AFRIKA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here