Home news PAMOJA NA KUANZA ‘KUSHAINI’ SIMBA…MORRISON ASHINDWA KUJIZUIA KUHUSU PABLO…AMSHUSHIA…

PAMOJA NA KUANZA ‘KUSHAINI’ SIMBA…MORRISON ASHINDWA KUJIZUIA KUHUSU PABLO…AMSHUSHIA…

 


STAA wa Simba kwa sasa,Mghana Bernard Morrison amesema ubora ambao anaonyesha katika kikosi hicho kwa sasa ni kutokana na majukumu ambayo amepewa na kocha wake mpya Pablo Franco.

Morrison alisema ratiba na mbinu ambazo anapewa mazoezini pamoja na kujituma kwake binafsi kumechangia kuwa kwenye ubora huo na lengo kubwa likiwa kuhakikisha Simba inafanya vizuri.

Alisema katika mazoezi kila mchezaji anapewa mbinu na jukumu lake la kwenda kufanya kwenye mechi ili kuaminiwa katika nafasi hiyo maana yake lazima ufanye vitu bora.

“Pengine hizo ndio silaha zilizofanya kuonekana kuwa bora zaidi wakati huu lakini si pekee yangu bali hata wachezaji wengine wote wa Simba ni hivyo hivyo,” alisema Morrison na kuongeza;

“Naamini nitaendelea kuboresha kiwango changu kuwa katika ubora huu ili kuona namna gani naipigania Simba kufanya vizuri katika mashindano haya ya kimataifa na kutetea vikombe vyote vya ndani,”

“Naamini kutokana na kikosi chetu kilivyo tunaweza kufanya vizuri zaidi ya sasa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika na Ligi Kuu Bara, ASFC na mengineyo kwani kila mchezaji anandoto za kulitimiza hilo.”

Kocha wa Simba, Pablo Franco alisema mara baada ya kufika katika kikosi cha Simba na kufanya mazoezi na wachezaji wote aligundua Morrison ni aina ya wale wachezaji spesho kutokana na aina yake ya uchezaji.

Pablo alisema Morrison hampi jukumu la kukaba bali akiwa na mpira anauwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi nyingi za kufunga kwa wengine, kufunga mwenyewe na kuwafanya mabeki wa timu pinzani muda wote kuwa makini nae.

Alisema muda ambavyo utazidi kuongezeka Morrison huyo wa wakati huu atakuwa bora zaidi kwani hata majukumu ndani ya kikosi kwa sasa amembadilishia na kutaka acheze kama mchezaji huru.

“Maana yake Morrison akicheza akiwa huru uwanjani atakuwa akitengeneza nafasi nyingi za kufunga kama ile ya Meddie Kagere, atafunga mwenye, mabeki watamchezea rafu na kupata penati au faulo ambazo tutazitumia kupata mabao,” alisema

“Naamini Morrison ni moja ya wachezaji hatari zaidi wakati tukiwa na mpira muda ambao tunashambulia ila kuna vitu vingine vya kiufundi nitamuongezea zaidi

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUFUNGWA NA YANGA JUZI....WATUNISIA WASEPA NA MAYELE...MCHONGO UKO HIVI...

“Ukiangalia katika kikosi changu kwa sasa ni Morrison tu ambaye ndio amekuwa bora bali hata wachezaji wengine wamezidi kuimarika kulingana na majukumu ya nafasi zao,”aliongeza Kocha huyo wa zamani wa Getafe na Real Madrid.