Home Habari za michezo MSEBIA ATUA MADEAMA

MSEBIA ATUA MADEAMA

Zikiwa zimepita siku tano tangu Medeama kuachana na Kocha Evans Adotey, jana Desemba 27 imemtambulisha Msebiar, Nebojsa Kapor.

Medeama iliachana na Adotey baada ya kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Yanga mechi ya nne ya hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wa Mkapa.

Kocha huyo (37) amesaini mkataba wa miaka miwili na mabingwa hao wa Ghana akiwa na leseni A ya Uefa na alishawahi kuifundisha timu ya Tena Youth na Benchem United za nchini humo.

Kapor ameshaanza kukinoa kikosi hicho huku akiwa na kibarua cha mchezo wa Ligi Kuu nchini humo dhidi ya Karela FC Desemba 30, 2023.

Medeama ipo kundi moja (D) pamoja na Yanga katika hatua ya makundi ya ligi ya Mabingwa Afrika na imesalia na michezo miwili dhidi ya Al Ahly na Belouizdad tu hatua hiyo.

Kundi hilo linaongozwa na Al Ahly ikiwa na pointi tano Yanga nafasi ya pili na pointi tano huku nafasi ya tatu ni CR Belouizdad mwenye pointi nne sawa na Medeama.

SOMA NA HII  CAF YAWAONGEZEA MCHEZAJI YANGA