Home Habari za michezo HIVI NDIVYO MORRISON ANAVYOIKAMUA YANGA SC ‘MIHELA’…KACHEZA MECHI 10 TU….

HIVI NDIVYO MORRISON ANAVYOIKAMUA YANGA SC ‘MIHELA’…KACHEZA MECHI 10 TU….

Morrison aikamua Yanga SC

Wakati Yanga SC ikijiandaa kuvuka maji kwenda Zanzibar kushiriki fainali za Kombe la Mapinduzi, Winga wake Mghana, Bernard Morrison yupo nchini kwao akiendelea na shughuli zake binafsi za kijamii huku namba zake tangu atue kwa Wanajangwani hao zikionekana kushitusha.

Morrison alirejea Yanga SC mwanzoni mwa msimu huu akitokea Simba na tangu ametua namba zake kwa maana ya mechi alizocheza, mabao na asisti zimeonekana kutombeba kulinganisha na wachezaji wengine wa timu hiyo lakini ni kama jamaa hawazi vile.

Morrison hadi sasa ameichezea Yanga SC mechi 10 tu za Ligi na kati ya hizo ni mchezo mmoja tu aliomaliza dakika zote 90, ambao ni ule wa duru ya kwanza dhidi ya Azam uliomalizika kwa sare ya 2-2 na baada ya hapo amekuwa hamalizi huku mara nyingi akitokea benchi.

Kwa ujumla, Morrison msimu huu hadi sasa ameichezea Yanga SC  dakika 543, ambazo ni chache ukilinganisha na wachezaji wengine wengi wa kikosi hicho.

Katika mechi hizo 10 alizocheza, amefunga mabao mawili tu, moja dhidi ya Coastal Union mechi ya pili ya ligi dakika ya nne na lingine ni lile la penalti dakika ya 45 alilofunga dhidi ya Geita Gold kwenye mzunguko wa kwanza pale CCM Kirumba Mwanza Yanga ikishinda kwa bao hilo hilo moja.

Mwamba huyo ametoa asisti tatu tu hadi sasa, moja ikiwa ile aliyompa Bakari Mwamnyeto akifunga bao la pili kwenye ushindi wa 2-0 mbele ya Polisi Tanzania katika mzunguko wa kwanza na nyingine alimpasia Jesus Moloko na kufunga bao la kwanza kwenye mechi dhidi ya Namungo katika ushindi wa 3-0.

SOMA NA HII  AUSSEMS ALALAMIKA KUFANYIWA UHUNI....ATOA KAULI ZA KASHFA...