Home Simba SC CHAMA NA LUIS WAPEWA MAJUKUMU KUELEKEA MBELE YA YANGA

CHAMA NA LUIS WAPEWA MAJUKUMU KUELEKEA MBELE YA YANGA


 KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes Da Rosa, kuelekea kwenye mechi yao dhidi ya Yanga, huku akiwa tayari ameshatoa majukumu maalum kwa nyota wake, Clatous Chama na Luis Miquissone.

 

Mei 8, mwaka huu, Simba itakuwa mwenyeji wa Yanga kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara baada ya ule wa mzunguko wa kwanza kumalizika kwa sare ya 1-1.

 

Simba inaingia kwenye mchezo huo ikiwa kinara wa Ligi Kuu Bara baada ya kukusanya pointi 61 zilizotokana na kucheza mechi 25, huku Yanga ikishika nafasi ya pili ikiwa na pointi 57.


Katika mchezo wa kwanza, Chama mwenye mabao saba na asisti 13, huku Luis akifunga mabao saba na asisti tisa, wote wawili hawakufunga mabao.


Yanga ilifunga kupitia kwa Michael Sarpong na Simba mfungaji akiwa Joash Onyango.Taarifa kutoka ndani ya kambi ya Simba iliyoanza Jumatatu, zinasema kwamba, Gomes ameanza kutoa majukumu kwa kila mchezaji wake akiwemo Chama na Luis.

 

β€œKila mchezaji amepewa majukumu yake siku hiyo, mbali na yote, lakini Luis ambaye anacheza winga, ametakiwa kurudi nyuma kusaidia ulinzi, pia kupeleka mashambulizi mbele ikiwezekana kufunga kabisa.

 

β€œChama yeye kazi kubwa siku hiyo ni kuhakikisha anamaliza majukumu yake yote ya kutuliza na kuanzisha mashambulizi, endapo wachezaji wakifuata kile ambacho wanaelekezwa na kocha, basi hao Yanga watakufa nyingi,” kilisema chanzo.


Kuhusu mchezi huo Gomes amesema kuwa anahitaji pointi tatu ili kuweza kutwaa ubingwa wa ligi.

SOMA NA HII  MAVITUZI YA OKRAH YAMPAGAWISHA KOCHA MSERBIA SIMBA...ABAKI AKICHEKELEA KOONI JINSI ATAKAVYOMTUMIA KUWALIZA...