Home kimataifa JOSE MOURINHO SASA NI MALI YA AS ROMA

JOSE MOURINHO SASA NI MALI YA AS ROMA


 KLABU ya AS Roma ya Italia imemtangaza  Jose Mourinho kuwa Kocha wake ikiwa ni wiki mbili tangu kibarua chake kiote nyasi akiwa Tottenham Hotspurs, aliyodumu nayo kwa muda wa miezi 17.

Mourinho (58) ambaye ni raia wa Ureno, amesaini kandarasi ya miaka mitatu na ataanza kuinoa AS Roma mwanzoni mwa msimu ujao.


Kocha huyo aliyewahi kufundisha Klabu za Porto, Chelsea, Real Madrid, Inter Milan na Manchester United, akiwa Tottenham alishinda michezo 45, kufungwa 24 na kutoka sare 17.

Baada ya mambo kuwa magumu ndani ya Ligi Kuu England anarejea ndani ya Serie A ambapo huko alifanya kazi kwa mafanikio alipokuwa huko. 

SOMA NA HII  BAADA YA KUAMBULIA ZA USO KOMBE LA DUNIA...WABRAZIL WAMTAKA GUARDIOLA...