Home Habari za michezo MAVITUZI YA OKRAH YAMPAGAWISHA KOCHA MSERBIA SIMBA…ABAKI AKICHEKELEA KOONI JINSI ATAKAVYOMTUMIA KUWALIZA…

MAVITUZI YA OKRAH YAMPAGAWISHA KOCHA MSERBIA SIMBA…ABAKI AKICHEKELEA KOONI JINSI ATAKAVYOMTUMIA KUWALIZA…

BAADA ya kuanza vizuri kampeni ya kusaka taji la Ligi Kuu Bara msimu huu kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Geita Gold juzi Jumatano, Kocha Mkuu wa Simba, Mserbia, Zoran Manojlovic ‘Maki’, amewasifu wachezaji wake kwa kiwango bora, huku akimvulia kofia kiungo Mghana, Augustine Okrah kwa kuweka wazi kiungo huyo atafunga sana msimu huu.

Okrah ambaye amesajiliwa na Simba kutokea kikosi cha Bechem ya Ghana, juzi Jumatano akiichezea Simba mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu alifanikiwa kuhusika kwenye mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-0 akifunga bao moja dakika ya 37, na kutengeneza penalti ya Chama dakika ya 85.

Kocha Maki alisema: “Nimefurahishwa sana na kiwango ambacho kimeonyeshwa na wachezaji wangu katika mchezo wetu dhidi ya Geita Gold, tulikuwa na wastani mzuri wa kufanya vizuri kutokana na nafasi za kufunga mabao ambazo tuliweza kutengeneza.

“Unaweza kuona mchezaji kama Okrah anaingia na kuonyesha uwezo mkubwa, nadhani kuendana na kipaji alichonacho kadiri muda utakavyokuwa ukiendelea, ataimarika zaidi na kufunga mabao mengi.”

SOMA NA HII  NABI ASHTUKIA JANJA JANJA YA WASAUZI...AFICHUA MTEGO AMBAO MAKOCHA WENGI WAMEUSHINDWA...