Home Habari za michezo MSIMU WA TUZO ZA SIMBA WARUDI KWA STAILI HII…SAFARI HII MASTAA WA...

MSIMU WA TUZO ZA SIMBA WARUDI KWA STAILI HII…SAFARI HII MASTAA WA KIMATAIFA WAANZA KUFUNGUA DIMBA…


MASTAA watatu wa kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Zoran Maki wametajwa kwenye kipengele cha kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki (Emirate Aluminium Simba ACP Fans Player of the Month).

Tuzo hizo zimerejea kwa mara nyingine tena baada ya ligi kukamilika kwa msimu wa 2021/22 na mabingwa kuwa Yanga huku Simba wakiwa ni washindi namba mbili.

Ni viungo watatu wamepenya kwenye orodha ya wachezaji ambao watapigiwa kura na mashabiki kuweza kupata tuzo hiyo.

Ni Clatous Chama raia wa Zambia, Pape Sakho raia wa Senegal na Sadio Kanoute raia wa Mali wote wakiwa ni viungo ndani ya kikosi hicho.

Kwa sasa Simba imeweka kambi nchini Sudan ambapo imealikwa kwenye mashindano maalumu na Klabu ya Al Hilal na mchezo wao wa kwanza walishinda mabao 4-2 dhidi ya Asante Kotoko.

Mchezo ujao unatarajiwa kuchezwa kesho Agosti 31 itakuwa dhidi ya wenyeji Al Hilal ya Sudan.

SOMA NA HII  KUDADEKI..SIMBA HII NI MAFIA SANA AISEE...WATUMIA TRIKI ZA KIJASUSI KUIPOKONYA KIUNGO WYDAD CASABLANCA...