Home Habari za michezo HIVI NDIVYO SIMBA WALIVYOCHEZA ‘KIJASUSI’ DILI LA MANZOKI KWENDA CHINA….NYUMA YA PAZIA...

HIVI NDIVYO SIMBA WALIVYOCHEZA ‘KIJASUSI’ DILI LA MANZOKI KWENDA CHINA….NYUMA YA PAZIA UKWELI WOTE HUU HAPA…


MABOSI wa Simba licha ya kujikausha, lakini ukweli walishtushwa sana waliposikia kwamba watani wao, Yanga wanamnyemelea Cesar Manzoki anayekipiga Vipers ya Uganda, hasa baada ya dili la kutaka kumleta kwenye dirisha la sasa la usajili kushindikana na fasta wakaamua kutumia akili kubwa.

Manzoki alisainishwa mapema mkataba wa awali wa miaka miwili na Simba kabla ya Vipers kuweka kauzibe ikitaka ilipwe Dola 200,000 ili kuvunja mkataba wa miezi miwili aliosaliwa nao, jambo ambalo mabosi wa Simba waliona ni fedha nyingi na kusubiri dirisha dogo wambebe kama mchezaji huru.

Hata hivyo, wakati wakiamini mambo yataenda freshi kwenye dirisha dogo zikaibuka taarifa kwamba Yanga walikuwa wakimvizia, kwani ilikuwa haijamaliza usajili na kuwashtua mabosi wa Simba ambao walimtuma mmoja wa vigogo wake kwenda kuzungumza upya na Vipers sambamba na Manzoki.

Baada ya kuona mambo yanaweza kutibuka, mabosi hao wakatengeneza mchongo wa maana wa kuzungumza na klabu moja ya China ili Manzoki aende huko kwa muda wa miezi minne hadi dirisha dogo wamrudishe na kumpa kazi kwenye kikosi kilichopo chini ya Kocha Zoran Maki.

Timu hiyo ya China iliyopewa nguvu na Simba ilifanikiwa kuwashawishi viongozi wa Vipers na kukubali kumuachia Manzoki aliyesainiwa huko kwa mkataba wa miezi minne.

Manzoki baada ya kwenda China, ikifika Desemba mkataba wake utamalizika na kuwa rahisi kuja Tanzania kuitumikia Simba inayomhitaji straika huyo wa mabao.

Akizungumza mapema Manzoki alisema viongozi wa Vipers wanafahamu mkataba wake unaisha baada ya miezi miwili kutoka wakati huu ila huo mkataba mwingine wa miaka miwili mbele wala hakuwa anautambua.

“Maamuzi yangu yatakuja kueleweka hapo awali kwani wakati huu kumekuwa na changamoto nyingi hadi kuamua kurudi Uganda kufanya mazoezi na Vipers,” alisema Manzoki ambaye katika kurasa zake za mitandao ya kijamii Manzoki aliandika ujumbe wa kuaga uliosomeka hivi;

“Wapendwa ni ngumu kwangu kupata maneno sahihi ya kusema kwaheri. Nithamini kumbukumbu nzuri na mafanikio katika miaka yangu miwili niliyokuwa hapa.”

SOMA NA HII  TIMU YA MSUVA KUSHUKA DARAJA...ACHEZA LIGI MOJA NA RONALDO...AMEZUNGUMZA HAYA

Ujumbe huo uliongeza kwa kusomeka;

“Kutoka chini ya moyo wangu asante Baba Lawrence Mulindwa, wachezaji wenzangu, uongozi, mashabiki na vyombo vya habari.”

Hata hivyo habari kutoka kwa mtu wa karibu wa mchezaji huyo mwenye uraia wa Afrika ya Kati, licha ya kuwa na asili ya DR Congo, alifichua kuwa, Manzoki anaenda China kama gia tu ya kukwepa kuitumikia Vipers iliyozuia dili lake la kuja Msimbazi mapema.

“Unajua wiki moja iliyopita alikuwa mmoja wa viongozi wa Simba, walizungumza na Manzoki na hata uongozi wa Vipers, lakini mambo kwa klabu yake ilikuwa ngumu, ndipo ikafanywa mipango aende kwamba China kwa dili la muda mfupi kabla ya kurejea Afrika moja kwa moja kuungana na Simba,” kilisema chanzo hicho kilichokataa kuandikwa jinja gazetini.

Juu ya ishu ya Yanga kumtaka, chanzo hicho kilisema hajawahi kuelezwa kama klabu hiyo inamtaka jambo mara kadhaa alikuwa akizungumza na Kocha Nasreddine Nabi anayefahamika naye kwa muda mrefu hata kabla ya kocha huyo kujiunga na Yanga mwaka jana.