Home Yanga SC YANGA WAENDELEA KUIVUTIA KASI SIMBA MDOGOMDOGO

YANGA WAENDELEA KUIVUTIA KASI SIMBA MDOGOMDOGO


 KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi raia wa Tunisia kimeendelea na mazoezi kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Mei 8.

Dakika 90 katika mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa timu zote zinahitaji kutwaa ubingwa wa ligi na mshindi atakuwa amejiweka kwenye mazngira mazuri ya kuelekea ubingwa ulipo.

Yanga kwenye msimamo ipo nafasi ya pili na pointi 57  baada ya kucheza jumla ya mechi 27 inakutana na Simba iliyo nafasi ya kwanza na pointi 61 baada ya kucheza jumla ya mechi 25.

Kwenye mchezo wao uliopita walipokutana Uwanja wa Mkapa, Novemba 7, Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Yanga 1-1 Simba.

Kwa Yanga alikuwa ni Michael Sarpong aliyetupia bao kwa mkwaju wa penalti na lile la Simba ni Joash Onyango aliyefunga kwa kichwa.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi zao zilizobaki ili waweze kufanya vizuri.

“Tupo tayari kwa ajili ya mechi zetu zijazo na tunahitaji kupata ushindi kwani kila kitu kipo sawa na maandalizi yanaendelea vizuri,” amesema.

Miongoni mwa nyota ambao wanapewa nafasi ya kuanza kwenye mchezo huo Mei 8 ni pamoja na kiungo mshambuliaji, Saido Ntibanzokiza raia wa Burundi. 

SOMA NA HII  GAMONDI AGÒMA KUZUNGUMZIA MECHI ZA KIMATAIFA AFUNGUKA HAYA