Home Yanga SC NCHIMBI: KUFUNGA MBELE YA GWAMBINA FC KUMENIONGEZEA HALI YA KUJIAMINI

NCHIMBI: KUFUNGA MBELE YA GWAMBINA FC KUMENIONGEZEA HALI YA KUJIAMINI


 NYOTA wa Yanga, Ditram Nchimbi ameweka wazi kuwa kufunga kwake bao mbele ya Gwambina FC kumemuongezea nguvu ya kuweza kujiamini zaidi kwa ajili ya mechi zinazofuata.

Mshambuliaji huyo mzawa hakufunga kwa muda wa mwaka mmoja jambo ambalo lilifanya mashabiki kumlalamikia kwamba hawezi kufunga.

Bao lake hilo alifunga mbele ya Gwambina FC, Uwanja wa Mkapa wakati wakishinda mabao 3-1.

Nchimbi ambaye kwenye mechi zote za Kariakoo Dabi za ligi amecheza anapewa nafasi ya kuanza katika mchezo ujao dhidi ya Simba, Mei 8.

Nyota huyo amesema:”Kufunga mbele ya Gwambina kwangu ni furaha na kunaongeza hali ya kujiamini kwa ajili ya mechi nyingine zijazo.

“Imani yangu ni kwamba ikiwa nitaendelea kupata nafasi itakuwa rahisi kwangu kufunga mabao mengi zaidi,” .

SOMA NA HII  ORODHA YA MAJINA YA WACHEZAJI YANGA WATAKAOSHIRIKI MASHINDANO YA KIMATAIFA