Home Habari za michezo SAFARI YA FEI TOTO DUBAI…SIRI IMEVUJA…TAJIRI ALIYEMSAFIRISHA HUYU HAPA…

SAFARI YA FEI TOTO DUBAI…SIRI IMEVUJA…TAJIRI ALIYEMSAFIRISHA HUYU HAPA…

Fei toto atimka Yanga SC

Baada ya sekeseke la kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ kuvunja mkataba na Yanga SC, ametimkia nje kwa mambo mawili – anatafutiwa kocha wa kumnoa ama timu ya kufanyia mazoezi pamoja na kupumzisha akili.

Fei aliipa Yanga SC Sh112 milioni kwa ajili ya kuvunja mkataba na timu hiyo.

Tangu ishu hiyo iibuke nyota huyo hajatoa kauli yoyote zaidi ya kuonyesha kwa vitendo kuondoka kambini, kisha akaonekana na timu ya JKU akicheza mechi ya kirafiki na jana ilitoka taarifa ametimkia majuu.

Juzi, Fei Toto kupitia mtandao wake wa kijamii aliandika “Alhamdulillah nimefika salama tayari kuanza majukumu yangu mapya.”

Chanzo cha ndani kimesema kuwa, Fei Toto mwenye mabao sita kwenye ligi amekwenda Dubai baada ya vigogo (jina tunalo) kumlipia kila kitu, ikiwemo kumtafutia kocha wa kumfundisha na timu ambayo atakuwa nayo kwa kipindi fulani wakati sekeseke hilo linapoa.

“Kwa namna vigogo wanavyompa heshima ya kipekee Fei Toto inamfanya apate nguvu kujiamini na kuona kipaji chake kinathaminiwa. Ukimuona hana wasiwasi wowote anajua maisha ya soka ni ya vipindi vinavyopita, hivyo ameamua kuutumia kisawasawa wakati wake.

“Huko nje ameenda kwa mambo mawili, kwanza katafutiwa kocha maalumu wa kumfundisha, pia anaweza akaonekana na timu za nje sijui ni ipi akifanya mazoezi, ili kuhakikisha anaendelea kuwa fiti.

“Fei Toto aliwaaga baadhi ya watu wake wa karibu lakini kukiwa na usiri mkubwa wa timu atakayojiunga kulinda kipaji chake na kocha gani aliyeandaliwa kumnoa,” kilisema chanzo chetu.

SOMA NA HII  MASHINE INGINE YA KAZI HII HAPA....SIMBA KUMLIPA MSHAHARA KUFRU..., BALEKE, PHIRI BYE BYE...