Home Habari za michezo RASMI…INONGA KUKOSEKANIKA SIMBA SC KWA ZAIDI YA WIKI ….

RASMI…INONGA KUKOSEKANIKA SIMBA SC KWA ZAIDI YA WIKI ….

Habari za Simba leo

Simba SC imethibitisha kuwa watamkosa kwa siku 10 Mlinzi wao mahiri, Henock Inonga Baka ambaye alipata majeruhi na kupelekea kuchanika sehemu ya mguu wake katika mchezo wao wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons SC kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo ambao Simba SC walipata ushindi mnono wa mabao 7-1 dhidi ya Maafande hao wa Jeshi la Magereza, Inonga aliumia na kushindwa kuendelea na mtanange huo baada ya kuchezewa ‘rafu’ mbaya na Mshambuliaji wa Prisons, Samson Mbangula.

Mshambuliaji Samson Mbangula alionyeshwa Kadi Nyekundu ya moja kwa moja (Straight Red Card) na Mwamuzi wa mchezo huo, Abdul Wajihi baada ya kucheza rafu hiyo kwenye mchezo huo uliopigwa Desemba 30, 2022 majira ya Saa 12:15 jioni.

Wakati Kikosi cha Wachezaji 30 wa Simba SC kikielekea visiwani Zanzibar kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi 2023, huenda Mlinzi huyo wa kati akakakosekana kabisa kwenye mashindano hayo ambayo yameanza kutimua vumbi Januari mosi, 2023 hadi Januari 13, 2023 visiwani humo.

SOMA NA HII  MO DEWJI ATEUA MABOSI WAPYA 21 SIMBA....KADUGUDA, MZEE DALALI NAO WAULA...