Home Uncategorized BRUNO APIGA MKWARA MZITO KWAMBA MOTO WAKE BADO SANA

BRUNO APIGA MKWARA MZITO KWAMBA MOTO WAKE BADO SANA


KIUNGO wa Manchester United, Bruno Fernandes amesema kuwa moto wake ndani ya klabu hiyo hautazima lazima afanye maajabu makubwa.

Nyota huyo ametwaa tuzo tatu ikiwa ni muda mfupi baada ya kujiunga na klabu hiyo ikiwa ni pamoja na tuzo ya Mchezaji Bora chaguo la wachezaji, (PFA), Tuzo ya Mchezaji Bora chaguo la Mashabiki wa Manchester United na juzi alisepa na tuzo ya mchezaji Bora wa Mwezi Februari ndani ya Ligi Kuu England.

Nyota huyo mwenye miaka 25 amecheza mechi tisa na kutupia mabao matatu ikiwa ni kwa penalti mbili na ametoa pasi nne za mabao.

“Tangu nilipokuwa mtoto nilikuwa natamani kucheza ndani ya Manchester United, kutua kwangu ndani ya Old Trafford ni ndoto iliyotimia nitafanya mambo makubwa na kazi bado inaendelea,’ amesema.

SOMA NA HII  KOCHA YANGA ASHTUKA, AWABADILISHIA MBINU PRISONS