Home Yanga SC YANGA WATUMA SALAMU BIASHARA UNITED

YANGA WATUMA SALAMU BIASHARA UNITED



UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba kuelekea kwenye mchezo wao Juni 25 dhidi ya Biashara United watapambana kupata ushindi.

Mchezo huo ni wa nusu fainali hatua ya Kombe la Shirikisho utakaochezwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi na mshindi wa mchezo huo atacheza kwenye fainali dhidi ya mshindi kati ya Azam FC v Simba.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na wataingia uwanjani kwa hesabu za kusaka ushindi.

“Mchezo wetu dhidi ya Biashara United ni muhimu kwetu na tunahitaji kushinda kwa namna yoyote ili kuweza kufikia malengo yetu ya kutwaa ubingwa.

“Kikosi kitawasili mapema Tabora ili kuweza kuwapa muda wa kupumzika wachezaji pamoja na kuwa tayaro kwa ajili ya mchezo huo,” amesema.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi imesepa Dar leo kuelekea Tabora.

SOMA NA HII  WAKILI YANGA:- "SIMBA INA WACHEZAJI WALIOZOEA KUMKABA RONALDO...AMEFUNGUKA HAYA