Home Makala ISHU YA ERIKSEN IWE FUNZO KWETU PIA, AFYA MUHIMU

ISHU YA ERIKSEN IWE FUNZO KWETU PIA, AFYA MUHIMU


 JAMBO la msingi kwa binadamu ni afya yake kuwa salama ili aweze kuendelea kupambana katika majukumu ya kila siku ambayo yanendelea.

 Kumekuwa na matukio ambayo yanatokea katika viwanja na wachezaji kupigwa na butwaa pamoja na mashabiki.

Suala la wachezaji kuanguka ghafla ama kupata matatizo ya kiafya ambayo yanawatokea pale ambapo wanakuwa katika majukumu yao uwanjani kusaka ushindi kwa ajili ya timu zao.

Hivi karibuni ulimwengu wa michezo ganzi ilitawala kwa muda baada ya kiungo wa Denmark, Christian Eriksen kuanguka na kupoteza fahamu kwenye mchezo wa Euro 2020 dhidi ya Finland ilikuwa ni Alhamisi.

Kwa jambo hili ambalo limetokea kwa wenzentu ambao wameendelea katika tenknolojia kuna jambo la kujifunza ili nasi pia tuweze kuendelea kuwalinda wachezaji wetu.

Ikumbukwe kwamba wachezaji wa timu ya taifa a Denmark walipigwa na ganzi kwa muda kisha wapo ambao walianza kumpa mchezaji huduma ya kwanza kwa sababu wana ujuzi katika kufanya hivyo.

Katika hilo ni muhimu pia hata ndani ya ardhi ya Tanzania wachezaji wakawa na ujuzi wa namna ya kutoa huduma ya kwanza.

Tumeona kwamba kuna matukio ambayo yamekuwa yakitokea ndani ya ligi kisha wachezaji wanapewa huduma ya kwanza kwa kusubiri watoa huduma ya kwanza.

Sio mbaya kwa yanayoendelea kwa sasa na hakuna ambaye anapenda kuona kwamba wachezaji wanaumia lakini jambo la muhimu ni tahadhari na kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzake.

Kumbuka namna ambavyo ilitokea siku ile kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula alipozimia uwanjani wakati walipokuwa kwenye mapambano dhidi ya JKT Tanzania.

Aliweza kuwahishwa hospitali akiwa kwenye gari la huduma ya kwanza na mwisho wa siku aliweza kurejea kwenye hali yake ya kawaida na sasa anaendelea na majukumu yake

Pia iliwahi kutokea nyakati za nyuma kwa mchezaji Emmanuel Okwi naye aliwahi kuzimia uwanjani wakati ule alipokuwa anacheza ndani ya Simba.

Naye pia alipewa huduma ya kwanza na watu wa huduma ya kwanza kisha maisha yakaendelea kama kawaida.

SOMA NA HII  ALICHOSEMA EDO KUMWEMBE KUHUSU UWEZO WA 'FEI TOTO'..ADAI NI YULE YULE TU..HANA JIPYA...

Jambo ambalo ningependa kwa wakati ujao na kwa mechi ambazo zimebaki Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) ambao ni wasimamizi wa masuala ya michezo Bongo wakatoa elimu kwa timu zote kuweza kujua namna ya kutoa huduma ya kwanza.

Ikiwa wachezaji watapewa elimu namna ya kutoa huduma ya kwanza itakuwa kazi rahisi katika kurahisha kutoa huduma ya kwanza kwa wachezaji wengine pale wanapopata matatizo.

Hakuna ambaye anaomba haya yatokee lakini tahadhari ni muhimu na maisha lazima yaendelee.

Pia wakati huu iwe ni somo kwa wachezaji kuzingatia katika kutunza afya zao na kuwa makini katika yale ambayo wanayafanya.

Timu pia zisiweke kando masuala ya kupima afya za wachezaji ni muhimu kwao pia kuweza kujua namna hali zao zinavyokwenda kila wakati.