Home Uncategorized KOCHA YANGA ASHTUKA, AWABADILISHIA MBINU PRISONS

KOCHA YANGA ASHTUKA, AWABADILISHIA MBINU PRISONS


Akijiandaa kuwavaa wapinzani wake Tanzania Prisons, Kocha Mkuu wa Yanga Mbelgiji Luc Eymael amesema mbinu alizozitumia katika michezo iliyopita waliyokutana hatazitumia tena na badala yake ataingia kivingine ili kuhakikisha anapata pointi tatu.

Kauli hiyo aliitoa kocha huyo ikiwa ni siku moja kabla ya kuvaana na Prisons, leo katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam saa 1 Usiku.

Katika mchezo huo, Yanga watakutana na ushindani mkubwa kutokana na kuwafunga Prisons mara zote mbili walizokutana kwenye ligi na Kombe la FA.

Luc alisema anatarajia kupata ushindani mkubwa katika mchezo huo kutokana na wapinzani wao kutokubali kupoteza kwa mara ya tatu mfululizo.

Luc alisema katika mchezo huo ataingia uwanjani na mbinu mbili tofauti za kuwavaa Prisons baada ya kuona moja waliyoingia nayo kushindwa kufanya kazi kutokana na wapinzani wao kuzisoma mbinu zao walipokutana.

Aliongeza kuwa hautakuwa mchezo mwepesi kwa kwao, lakini kutokana na maandalizi aliyoyafanya kwa kuboresha safu yake ya ulinzi na ushambuliaji anaamini atapata ushindi, kikubwa mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani.

“Katika msimu huu tumekutana mara mbili na Prisons, hivyo tunaamini tayari wamezijua mbinu na mifumo tunayoitumia, hivyo basi kama kocha tutaingia kwa tahadhari kubwa katika pambano hili.

“Kikubwa tutaingia kwa mbinu mbili na tutazibadilisha baada ya kuona tulioingia nayo wapinzani kuijua, hivyo haraka tutabadilisha na kutumia nyingine mpya ambayo ninaamini itatupa ushindi.

“Mchezo huu siyo mwepesi kwetu, kwani wapinzani wetu hawatakubali kufungwa kwa mara ya tatu mfululizo ni lazima waje kivingine na kutuzuia kupata ushindi hapa nyumbani, hivyo tumejiandaa katika hilo,” alisema Luc.
SOMA NA HII  VIKOSI VINNE VILIVYO KUNDI LA TAIFA STARS, ANGALIA UTUAMBIE UNAAMINI KIPI NI KIKOSI BORA KWA NAMBA, YAANI 1, 2, 3, NA 4