Home Uncategorized KAMBI YA TIMU YA JKT TANZANIA YAVUNJWA RASMI LEO

KAMBI YA TIMU YA JKT TANZANIA YAVUNJWA RASMI LEO

UONGOZI wa Klabu ya JKT Tanzania, leo Machi 18,2020 rasmi umevunja kambi yake kutokana na maelekezo yaliyotolewa jana na Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu Kasim Majaliwa kuhusu zuio la kuwepo kwa mikusanyiko mbalimbali kutokana na kuwepo ugonjwa wa Corona hapa nchini.

Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa JKT Tanzania , Jamila Mutabazi imeeleza kuwa wachezaji wote wanarejea nyumbani kuanzia leo.

Pia wachezaji wametakiwa kuendelea kujikinga na kufuata maelekezo yanayotolewa na Serikali sambamba na wataalam wa afya.

SOMA NA HII  VPL: YANGA 1-1NAMUNGO