Home Uncategorized SIMBA YAIPOTEZEA YANGA LIGI YA MABINGWA JUMLAJUMLA

SIMBA YAIPOTEZEA YANGA LIGI YA MABINGWA JUMLAJUMLA


BEKI wa Simba, Pascal Wawa, amefunguka kuwa kwa sasa wapinzani wao wakiwemo Yanga wanatakiwa kusahau juu ya kushiriki katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao kwani hawataweza kuufikia ubingwa wa msimu huu. –

Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 71 huku ikibakiza mechi 10 kumaliza Ligi Kuu Bara, tofauti na Yanga iliyo katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 51 wakati imebakiza mechi 11 kabla ya kumaliza ligi. –

Akizungumza na Championi Jumatano, Wawa alisema kuwa mbali ya Yanga, hakuna timu yoyote itakayoweza kufikia pointi zao kwa sasa huku akisisitiza wanataka kushinda mechi zao zote zilizobakia.

SOMA NA HII  KOCHA STARS: UWEZO WA WACHEZAJI UNAONGEZEKA KILA SIKU