Home Uncategorized KOCHA STARS: UWEZO WA WACHEZAJI UNAONGEZEKA KILA SIKU

KOCHA STARS: UWEZO WA WACHEZAJI UNAONGEZEKA KILA SIKU


KAIMU Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Ettiene Ndayiragije amesema kuwa uwezo wa wachezaji unaongezeka kila siku kadri wanavyafanya mazoezi.

Stars ipo kwenye maandalizi ya kujiandaa na mchezo wa CHAN dhidi ya Kenya utakaochezwa Julai 28, Uwanja wa Taifa, saa 10 Jioni.

“Nawatazama kwa ukaribu wachezaji wote na ninapata muda wa kuzungumza nao kila mmoja jambo ambalo linanipa mwanga wa kujua kile ambacho wanafikiria.
“Imani yangu ni kwamba kadri tunavyozidi kufanya mazoezi ndivyo ambavyo tunazidi kuimarika na malengo yetu ni kufanya vizuri hivyo mashabiki watupe sapoti,” amesema

SOMA NA HII  MORRISON: NINGEPANDA NDEGE INGEKUWA DHARAU KWA WENZANGU...