Home Habari za michezo KISA SIMBA ‘KUFELI’ MSIMU HUU….CHAMA AMTUPIA LAWAMA KOCHA MRAZILI…ADAI YEYE NDIO CHANZO..

KISA SIMBA ‘KUFELI’ MSIMU HUU….CHAMA AMTUPIA LAWAMA KOCHA MRAZILI…ADAI YEYE NDIO CHANZO..

Habari za Simba

Kiungo Mshambuliaji wa Simba, Clatous Chota Chama, amefungukia sababu kubwa ambayo imefanya wapotee msimu huu na kuwafanya wakose kila kitu.

Chama ambaye anawania Tuzo ya Kiungo Bora wa Ligi Kuu Bara msimu huu sambamba na Bruno Gomes, Mzamiru Yassin, Stephane Aziz Kin a Saidi Ntibazonkiza, amesema moja ya kitu kilichowaumiza msimu huu unaoenda ukingoni walikuwa wakifanya sana mabadiliko katika kikosi chao na kupelekea kukosa uwiano mzuri.

Kiungo huyo raia wa Zambia, alisema hilo ni jambo baya sana kwao ingawa huwa inatokea kwenye mchezo wa mpira wa miguu.

“Msimu unakwenda ukingoni na tupo tunafanya maandalizi ya mechi za mwisho. Kuhusu kufanya vibaya msimu huu ni mabadiliko ya kikosi mara kwa mara.

“Mwalimu alikuwa anafanya ‘rotation’ nafikiri hiyo ilikuwa sababu ya kuwa na matokeo ya kubadilikabadilika kwa kuwa tulikuwa tunakosa uwiano,” alisema Chama.

SOMA NA HII  MGUNDA:- KAMA MATUSI YA KAMWE NI ILI YANGA ISHINDE BASI SAWA...ILA WASIPOSHINDA KESHO....