Home Uncategorized KAGERE ATAJA ANACHOKIPENDA KUKIFANYA AKIWA NDANI YA UWANJA

KAGERE ATAJA ANACHOKIPENDA KUKIFANYA AKIWA NDANI YA UWANJA


MEDDIE Kagere, mshambuliaji wa Simba amesema kuwa furaha yake ni kufunga na atakuwa akifanya hivyo kila akipata nafasi.


Kagere ni kinara wa utupiaji ndani ya Ligi Kuu Baa akiwa ametupia mabao 19 akikimbizana na wazawa kama Relliants Lusajo, Yusuph Mhilu wenye mabao 11.

“Ninapenda kutimiza majukumu yangu nikiwa ndani ya uwanja, nikipata nafasi ya kufunga nitafunga kwani hakuna kazi nyingine ninayotakiwa kuifanya kutokana na nafasi yangu,”.

Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 71 huku kwa upande wa mabao ikitupia mabao 63.
SOMA NA HII  CORONA KWA KOCHA ARSENAL, BEKI JUVENTUS NI UJUMBE HADI LIGI KUU BARA