Home Uncategorized LICHA YA KUSEPA NA POINTI TATU, POLISI TANZANIA YAKIRI KUBANWA NA NDANDA

LICHA YA KUSEPA NA POINTI TATU, POLISI TANZANIA YAKIRI KUBANWA NA NDANDA

MALALE Hamsini, Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania amesema kuwa ushindi walioupata mbele ya Ndanda FC haujamfurahisha kutokana na kuzidiwa mbinu na wapinzani wake.

Polisi Tanzania ilisepa na pointi tatu mazima mbele ya Ndanda kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa jana, Machi 14 Uwanja wa Ushirika kwa bao 1-0.

Bao pekee la ushindi lilifungwa na Marcel Kaheza dk ya 13 kwa mkwaju wa penalti lilidumu mpaka dk 90 za mchezo ambapo jitihada za Ndanda FC kuweka mzani usawa ziligonga mwamba.

“Tumeshinda na kupata pointi tatu lakini hatukuwa kwenye ubora wetu, tulizidiwa mbinu na wapinzani jambo ambalo ni lazima tulifanyie kazi,” amesema.

Ushindi huo unaifanya Polisi Tanzania kwa nafasi ya sita ikiwa na pointi 45 imecheza mechi 29 huku Ndanda ikiwa nafasi ya 15 na pointi 31.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA GAZETI LA SPOTI XTRA KATIKA UKURASA WA MBELE LEO JUMAPILI