Home Burudani BAADA YA MANARA…MWIJAKU NAYE MASHUSHIA MVUA YA MANENO MWAKINYO…ADAI NI MUONGO…AFICHUA YA...

BAADA YA MANARA…MWIJAKU NAYE MASHUSHIA MVUA YA MANENO MWAKINYO…ADAI NI MUONGO…AFICHUA YA PROMOTA WAKE…


DC wa Insta, Mwijaku amefunguka na kusema kwamba bondia Hassan Mwakinyo amewadanganya Watanzania kwamba kuna pambano la marudiano kati yake na bondia Liam Smith wa Uingereza, Januari 23, 2023.

Mwijaku ameyasema hayo huku akionyesha video anayodai kuwa ametumiwa na promota wa pambano hilo wakati alipokuwa akilalamika kuhusu pambano hilo lilivyomalizika na kuongeza kwamba ametumia nguvu kubwa na pesa katika kuandaa pambano hilo akiamini kwamba litakuwa la aina yake na badala yake haikuwa kama alivyotarajia baada ya Mwakinyo kushindwa kucheza.

Aidha, Mwijaku amedai kuwa hata promota mwenyewe amekasirishwa na kitendo hicho cha Mwakinyo na kudai kuwa hakuna pambano la marudiano na kwamba hakuna pambano ambalo linachezwa siku ya Jumatatu katika nchi za Ulaya.

Pambano la Mwakinyo lilipigwa usiku wa Septemba 3, 2022 ambapo Mwakinyo alishindwa kuendelea na pambano hilo na refa kulazimika kulimaliza raundi ya nne baada ya Mtanzania huyo kudai kuwa viatu vilikuwa vikimbana na kumsababishia maumivu, hivyo akampa ushindi wa TKO Smith.

“Ulituomba tukuombee, sisi kama Watanzania tukafunga na kusali tukaomba, halafu mwisho wa siku pambano unakuja kuliuza kilaini vile. Promota amenitumia DM, ameonyesha kukasirishwa na amesema Mwakinyo ni mwongo hakuna pambano la marudiano na amechukizwa na alichofanya Mwakinyo.

“Unadanganya kiatu kimabana, kitakubana vipi? Ujinga ule. Ulaya hakuna mambo ya kusahau mabegi wewe, Ulaya haipo hiyo, ataje kampuni ya ndege. Mimi ni mwandishi nina haki ya kumhoji,” amesema Mwijaku.

SOMA NA HII  WAKATI WATU WAKIMUONA 'CHENGA' KWA VITUKO VYAKE...UKWELI NI KWAMBA HAKUNA SIMBA BILA MORRISON..