Home Habari za michezo KISA MECHI NA AZAM….KISUBI AMUONDOA DIARA YANGA….AMTAKA ASEPE BONGO HARAKA…

KISA MECHI NA AZAM….KISUBI AMUONDOA DIARA YANGA….AMTAKA ASEPE BONGO HARAKA…


Kipa wa Polisi Tanzania, Jeremiah Kisubi amemshauri mdaka mishale wa Yanga, Djigui Diarra akapumzike kwao ili kuupa mwili wake nguvu ya kufanya kazi kwa ushindani mkali.

Kisubi ameufafanua ujumbe alioundika kwenye mitandao ya kijamii, akimtaka Diarra akapumzike kwao ila anachoshangaa ni tafsiri za baadhi ya watu ambao wanauhusisha ujumbe huo na imani za kishirikina.

“Msimu uliopita ukitaja makipa wenye viwango vya juu, aliyekuwa anaongoza ni Diarra, anajua kuituliza timu, anatoa pasi za mwisho, jambo ambalo limeleta chachu kwa makipa wa Ligi Kuu Bara, ila msimu huu kaanza na kiwango cha chini.” amesema Kisubi.

Kisubi ambaye alisajiliwa Simba na kutoka Tanzania Prisons hakucheza mechi hata moja, kisha akapelekwa kwa mkopo Mtibwa Sugar alikokiri hakucheza vizuri, kutokana na changamoto ambazo alikuwa anakabiliana nazo, amesema anapenda kuona makipa wanashindana kwa uwezo ndio maana haoni wivu kumshauri Diarra.

“Hata kama hatakwenda kupumzika kwao, atafute sehemu nyingine ambako akakae angalau wiki bila kujishughulisha na mambo ya soka, akili yake itarudi mchezoni, lakini hawezi kupumzikia kwenye timu wakati yeye ni kipa namba moja, kocha atampanga tu,” amesema.

Kisubi ambaye aliumia kidole akiwa kwenye maandalizi ya msimu na ameanza mazoezi ana siku nne tangu atoke kuuguza majeraha, amesema kipa mwingine wa kigeni ambaye alikuwa anafanya vizuri ni Razak Abalora ambaye anafananisha uwezo wake na Diarra.

“Wachezaji ni binadamu, tuna familia zinazotutegemea kuna wakati mwingine tunaweza kuzidiwa na mawazo, lakini ukipata muda wa kupumzika akili inarejea upya kazini, napenda aina ya uchezaji wake ndio maana sitamani aendelee na kiwango alichoanza nacho msimu huu,”amesema.

SOMA NA HII  UTAMU WA MECHI YA LEO UKO KWA MASTAA HAWA....AKIPWAYA MMOJA TU GAME IMEISHA KWAKE...