Home news SAKHO AZIDI KUIPAISHA SIMBA KIMATAIFA …GOLI LAKE LAPENYA KWA UBORA AFRIKA…

SAKHO AZIDI KUIPAISHA SIMBA KIMATAIFA …GOLI LAKE LAPENYA KWA UBORA AFRIKA…


PAPE Sakho kiungo mshambuliaji wa Simba bao alilowatungua RS Berkane limechaguliwa kuwa bao bora la wiki katika mashindano ya Kombe la Shirikisho.

Pape alipachika bao hilo Uwanja wa Mkapa, Machi 13 wakati Simba ikivuna pointi tatu mazima.

Ilikuwa dakika ya 44 Sakho alifanya hivyo baada ya kupokea pasi kutoka kwa Meddie Kagere.

Kabla ya kufunga bao kiungo huyo alisepa na kijiji cha mabeki na walikuwa na hofu ya kumkata buti kwa kuwa alikuwa ndani ya 18.

Ikumbukwe kwamba hata bao lake la kwanza mbele ya ASEC Mimosas la mtindo wa Acrobatic nalo lilichaguliwa kuwa bao bora.

SOMA NA HII  RASMI..MTIBWA SUGAR YAMALIZANA KIBABE NA DEO KANDA...ISHU NZIMA ILIKUWA HIVI...