Home Uncategorized AZAM FC V MBEYA CITY HAPATOSHI,TAMBO ZATAWALA

AZAM FC V MBEYA CITY HAPATOSHI,TAMBO ZATAWALA


BAADA ya matajiri wa Dar es Salaam,  Azam FC kugawana pointi mojamoja na Lipuli kwenye mchezo wao uliochezwa Uwanja wa Samora, hesabu zao ni mbele ya Mbeya City.

Azam FC inayonolewa na Aristica Cioaba ilikubali sare ya kufungana bao 1-1 mbele ya Lipuli, mchezo uliochezwa Julai 19.

Ushindi huo umeifanya ibaki nafasi ya tatu ikiwa na pointi 66 ikiachwa na Yanga kwa tofauti ya pointi mbili.

Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 68 zote zimecheza jumla ya mechi 36 ndani ya Ligi Kuu Bara na hesabu zao wote ni kuona wanamaliza wakiwa nafasi ya pili.

Azam FC inakutana na Mbeya City ambayo inapambana kubaki ndani ya ligi hivyo utakuwa ni mchezo wenye ushindani mwanzo mwisho.

Mbeya City iliyo chini ya Amri Said ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 42 ambazo hazimpi uhakika wa kubaki ndani ya ligi ikiwa atapoteza Uwanja wa Azam Complex. 

Ofisa Habari wa Azam FC,  Zakaria Thabit amesema wanahitaji ushindi na kikosi kipo tayari kwa ushindani.

Ofisa Habari wa Mbeya City,  Shaha Mjanja amesema kuwa kila kitu kipo sawa wanahitaji pointi tatu.

SOMA NA HII  MUONEKANOWA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA