Home Habari za michezo KUELEKEA MECHO NA MAMELOD…..AUCHO MDOGO MDOGO AANZA KUZIPANGA GIA

KUELEKEA MECHO NA MAMELOD…..AUCHO MDOGO MDOGO AANZA KUZIPANGA GIA

Habari za Yanga

Kiungo wa Yanga, Khalid Aucho amesema anaendelea vizuri na yupo kwenye hali nzuri ya utimamu wa mwili huku akiwaambia mashabiki wa klabu hiyo kuwa, amewasikia na kuwataka watulie kabla ya kurejea uwanjani kuwapa burudani mbele ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Yanga inatarajiwa kuwa wenyeji wa Mamelodi, Jumamosi ijayo katika mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Aucho aliyekuwa majeruhi akiwapa matumaini makubwa sambamba na winga Msauzi, Skude Makudubela aliyesema Kwa Mkapa lazima mtu apigwe.

Tuanze na Aucho. Kiungo huyo aliye injini wa Yanga kwa sasa katika eneo la kiungo, ameliambia Mwanaspoti kwamba amekuwa akisikia presha waliyonayo mashabiki tangu taarifa za kufanyiwa upasuaji wa goti zilipotolewa, lakini akawaambia watulie kwani hali yake kwa sasa inaendele vyema.

Aucho alisema amefurahi kuona tayari ameanza mazoezi chini ya kocha wa utimamu wa mwili (Fitness coach), ikiwa ni ishara njema ya kurudi tena uwanjani kuipambania timu katika mechi zilizopo mbele yao ikiwamo hiyo ya Mamelodi itakayopigwa Jumamosi ijayo kuanzia saa 3:00 usiku.

“Siku sio nyingi nitarejesha furaha kwa mashabiki wa Yanga natambua wamekuwa wakiniombea nirejee haraka, hiyo ndio raha yao hivyo na mimi nawaambia kuwa nimeanza mazoezi na dua zao zimesikika na hofu yaop imeondola na sasa watulie wajiandae kuwapa furaha muda sio mrefu,” alisema Aucho, raia wa Uganda.

“Jukumu la kuzungumza ni lini narudi uwanjani nawaachia madaktari waliosimama nami kwa ajili ya kuhakikisha narudi katika haliya kawaida kauli yangu ni kwanza naendelea vizuri nimepita kwenye hatua zote muhimu na hali yangu imeimarika na kilichobaki ni kupiga kazi tu,” aliongeza Aucho.

Aucho alifanyiwa upasuaji mdogo wa goti uliothibitishwa na daktari wa klabu hiyo, Moses Etutu, ambaye awali alikuwa na wasiwasi kwa kiungo huyo kukaa nje kwa muda wa wiki tatu lakini kutokana na mapokeo ya mgonjwa ameweza kuwa na maendeleo mazuri tofauti na matarajio yao.

Kiungo huyo aliumia katika mechi ya mwisho ya makundi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya watetezi Al Ahly iliyopigwa Cairo Misri na Yanga kulala 1-0, hivyo kuikosa micheo mitatu ya Ligi Kuu ikiwamo dhidi ya Namungo, Geita Gold na Azam FC

SOMA NA HII  AMBOKILE APEWA MWEZI MMOJA NKANA